Waziri mkuu wa
Benin, Lionel Zinsou, anasemekana kuwa salama baada ya ndege ya
helikopta alimokuwa akisafiria, kuanguka ilipokuwa ikitua kaskazini mwa
nchi hiyo.
Ofisa mmoja wa serikali amesema kuwa helikopta hiyo,
ilianguka ilipokuwa katika harakati za kutua, katika uwanja mmoja wa
michezo mjini Djougou.Kiongozi huyo alikuwa amepangiwa kuhutubia mkutano wa hadhara.
Kilichosababisha ajali hiyo hakijajulikana hadi sasa.
Bwana Zinsou aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwezi Juni, na ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari mwakani.
Post a Comment