0

Bado hali sio nzuri ndani ya klabu ya Man United, haikatishi siku bila mitandao ya kijamii, magazeti na tovuti kujadili juu ya kibarua cha kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal, mengi yameandikwa na kwakuwa Uingereza ndio Ligi inayopendwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo vina nguvu, basi usishangae kuona nakuletea stori nyingine kutoka Man United.
2F82FA9000000578-3373134-Manchester_United_were_beaten_2_0_at_home_by_Norwich_at_Old_Traf-m-22_1450958731621
December 24 nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney amefunguka kuhusu wachezaji wenzake wanavyowaza namna ya kupambana na kuokoa kibarua cha kocha wao Louis van Gaal ambaye anatajwa kuwa katika wakati mgumu, na kama timu yake ikifanya vibaya katika mchezo dhidi ya Stoke City ndio atakuwa katika wakati mgumu zaidi.
“Kiukweli kuna watu wengi ambao wanazungumza na kuandika vitu ambavyo havipo au wanaamini vinaweza kutokea, watu wanaandika vitu ambavyo kiukweli hawavijui. Kwa sasa tunajitahidi na tunapambana kubadilisha mambo yalivyo kwa ajili ya kocha wetu, ni muhimu kuungana kwa pamoja” >>> Wayne Rooney
2F8297E500000578-3373134-image-a-30_1450959456365
Louis van Gaal
Stori zinazodaiwa zilitoka kwa baadhi ya wachezji wa Man United zilinukuliwa kuwa, wachezaji hawana mahusiano mazuri na kocha Louis van Gaal katika vyumba vya kubadilishia nguo sambamba na wachezaji kukosa mzuka wa kucheza, maneno ambayo kwa mujibu wa kauli ya Rooney, inaashiria kuwa sio kweli ni mambo yanayoandikwa.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top