25 wateketea katika hospitali Saudi Arabia
Takriban watu 25
wameuwa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto katika hospitali
moja iliyo mji wa Jazan nchini Saudi Arabia.
Moto huo ulitokea
katika gorofa ya pili ya hospitali ya jazan ambapo vyumba vya kujifungua
na vile vya wagonjwa mahututi vipo mapema leo Alhamisi .Walionusurika na majeruhi wamehamishwa kupelekwa katika hospitali zingine.
Haijabainika kile kilicho sababisha moto huo na sasa uchunguzi unandelea .
Picha za tukio hilo zilizochapishwa kwenye jarida la kila siku la Okaz zinaonesha mabaki ya hospitali hiyo yaliyotekekea na kuharibika kabisa.
Mji wa wa Jazan uko karibu na mpaka wa Saudia na Yemen taifa ambalo limesakamawa na vita kati wenyewe kwa wenyewe.
Mapema mwezi huu kombora lililokuwa likielekea Jazan lilidunguliwa na majeshi ya Saudia hata hivyo hivyo haijabainika kufikia sasa iwapo moto huo unauhusiano wowote na mapigano yanayoendelea huko Yemen.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.