Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litafunguliwa mwezi January ili kuvipa fursa baadhi ya vilabu kufanya usajili wa wachezaji kuimarisha vikosi vyao katika ligi mbalimbali ili kutafuta mafanikio au kufanya vizuri kwenye ligi hizo.
Kuna wachezaji na makocha mbalimbali wamekuwa wakitajwa au kuhusihwa na usajili huo unaosubiriwa na wadau wa soka kuona timu wanazozi-support zitafanya nini muda huo ukifika.
Hii hapa top 5 ya majina ya wachezaji na makocha yanayotajwa sana kwa sasa yakihusishwa kujiunga au kutemwa na baadhi ya vilabu.
5. Manchester United yamuonya Louis Van Gaal
Ripoti kutoka ndani ya Old Trafford zinasema kwamba uongozi wa juu wa Manchester United haufurahishwi na namna ambavyo kocha mkuu wa timu hiyo Lois van Gaal anavyopambana kufuzu kutoka kwenye makundi kwenda hatua ya 16 bora ya michuano ya mabingwa Ulaya.
Mholanzi huyo ameambiwa kuwa viongozi hao wa United hawataki kukiona kikosi chao kikenguliwa kwenye michuano hiyo katika hatua za mapema wakati kikosi hicho kikijiandaa kwa ajili ya mechi ya kufa na kupona dhidi ya Wolfsburg wiki hii.
4. Arsenal yatakiwa kumsajili Wanyama
Akiwa kwenye ziara yake nchini Kenya mkongwe wa Arsenal, Robert Pires ameushauri uongozi wa timu yake ya zamani kumsaini kiungo wa Southampton Victor Wanyama.
Anaamini kwamba, mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya ni ‘world-class material’ na amemshauri kocha Arsene Wenger kumsaini mchezaji huyo.
3. Man United yamtaka Kane
Ripoti kutoka London zinasema kwamba, manager wa Manchester United Louis van Gaal yukotayari kumsajili striker wa Tottenham Hotspur Harry Kane kama target man striker wake. Mchezaji huyo ataigharimu United kitita cha pauni milioni 50.
2. Mourinho huenda akatimuliwa endapo atafungwa na FC Porto
Taarifa kutoka Stamford Bridge zinasisitiza kwamba, Jose Mourinho huenda akatimuliwa ikiwa atapoteza mchezo wa klabu bingwa dhidi ya FC Porto Jumatano hii.
Taarifa hizo ambazo si rasmi zimekuja siku siku mbili baada ya The Blues kupokea kichapo cha nane kwenye ligi ya England kutoka kwa Bournemouth timu ambayo ipo kwenye hatari ya kushuka daraja.
1. Guardiola yuko tayari kuisubiri Manchester United
Manager wa Bayern Munich Pep Guardiola inaripotiwa amewaambia watu wake wa karibu kuwa yuko tayari kusubiri hadi 2017 ambapo mkataba wa kocha wa sasa Louis van Gaal utakapokuwa unamalizika ili ajiunge na Manchester United.
Taarifa za awali zilikuwa zinadai kuwa ‘mashetani wekundu’ walikuwa tayari kumtimua mholanzi huyo majira ya kiangazi ili kutengeneza mazingira ya kumnasa kocha huyo wa zamani wa Barcelona lakini mambo yalibailika siku chache baadae.
Post a Comment