Ligi Kuu ya soka
ya England iliendeela tena jana usiku kwa mchezo mmoja katika dimba la
Goodson Park ambapo Wenyeji Everton waliwaalika Crystal Palace na
kutoka sare ya bao 1-1.
Kwa matokeo hayo Crystal Palace sasa imekwea hadi nafasi ya 6, wakiwa na Pointi 23, na Everton wakiwa Nafasi ya 9 wakiwa na pointi 22 .
Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena Jumamosi Desemba 12 kwa michezo kadhaa ambapo Norwich itawaalika Everton, Crystal Palace watakuwa wenyeji wa Southampton, Man City dhidi ya Swansea, Sunderland itaikabili Watford, West Ham watawaalika Stoke na Bournemouth watakuwa wenyeji wa Manchester United.
Post a Comment