0
Kocha wa Mbeya City Abdul Mingange
Kocha wa Mbeya City Abdul Mingange
Kocha mkuu wa Mbeya City Meja mstaafu Abdul Mingange ambaye amekabidhiwa kikosi hicho hivi karibuni ameweka wazi mipango yake baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi kutimkia kunako klabu ya Yanga
Mtandao huu umezungumza na Mingange kutaka kujua mipango yake ni ipi baada ya yeye kukabidhiwa jahazi la kuiongoza timu hiyo ambayo msimu huu haijanza vyema mbio za ligi tofauti na misimu miwili iliyopita.
“Malengo yanafahamika ni yaleyale kwa kila klabu kufanya vizuri kwenye ligi na kuleta jina lake liwe juu kama misimu miwili iliyopita na hiyo hasa inaweza ikafanikiwa ikiwa ushirikiano kati yangu na benchi zima la ufundi pamoja na viongozi utakuwa ni mzuri. Na hiyo tayari imeanza kuonesha picha nzuri kwani tayari nimefanikiwa kusajili wachezaji wawili watatu”, amesema Meja mstaafu Abdul Mingange.
“Wako wachezaji wanne ambao tunataka kuwasajili na mipango inaenda vizuri wachezaji ambao tumeshakamilisha usajili wao ni Abdallah Juma kutoka Toto Africans na Tumba Swed kutoka Coastal Union ya Tanga”.
Kuhusu mipango ya Mbeya City kwenye ligi ambayo inatarajiwa kuendelea December 12 Mingange anasema kwamba, tayari wameshacheza michezo kadhaa ya kirafiki na Tukuyu Stars pamoja na Kombaini ya Kyela kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya Vodacom Tanzania bara.

Post a Comment

 
Top