Rais Dkt.Magufuli Atangaza Baraza LA Mawaziri ambalo amelitaja kuwa ni Dogo na lenye tija ikiwa ni kubana matumizi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo
Desemba 10, 2015.
Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi
punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi
wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na
baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na
manaibu waziri.
Magufuli: Kumekuwa
na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua
baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa
tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.
Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na
mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi
kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na
kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya
wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.
Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na
effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri
watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na
semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au
kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.
BARAZA LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora
Mawaziri – George Simbachawene na Angela Kairuki
Naibu Waziri – Sumeilam Said Jaffo
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Joelson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri – William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – Prof. Mwijarubi Muhongo
Naibu Waziri – Medard Kalemani
Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri – Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Waziri – Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – William Lukuvi
Naibu Waziri – Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage
Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Ummy Mwalim
Naibu Waziri – Dkt. Hamis Kigwangalla
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Nape Nnauye
Naibu Waziri – Anastasia Wambura
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela
Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?
Magufuli: Niliyowachagua
wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na
ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana
hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.
Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?
Magufuli: Wewe
ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu
huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa
tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa
kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi
mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka
kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa
na baraza la watu 34 tu.
Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi
tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina
elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.
Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo
wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa,
contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua,
Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi
tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote
tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.
Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharejesha zile hela?
Magufuli: Swali hilo kamuulize kamishna wa kodi TRA.
SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?
Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.
Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?
Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.
Asanteni sana na ninawashukuru
VIDEO HII HAPA CHINI
VIDEO HII HAPA CHINI
Post a Comment