Wanachama wa tume ya uchaguzi Zanzibar, ZEC
Waangalizi wa
uchaguzi mkuu wa ndani nchini Tanzania TEMCO wamesema kuwa wanashangazwa
na hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kudai kuwa uchaguzi
visiwani humo haukuwa huru na haki.
Mwenyekiti wa TEMCO Dr Bennson
Bana anasema kuwa amesema kuwa kwa mjibu wa waangalizi wao waliokuwa
katika vituo vitu mbalimbali visiwani humo walijiridhisha na hatua za
uchaguzi huo pamoja na kwamba mwisho wa siku uchaguzi huo ukafutiliwa
mbali na tume.Bana pia amesema kuwa TEMCO ilishtushwa na tamko la octoba 26 2015 lililokuwa lililosomeka kuwa CUF yashinda uchaguzi wa kihistoria Zanzibar.
Msimamo wa TEMCO ni kuisihi tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufikiria upya umamuzi iliyoufikia,lakini wamevishauri vyama vya siasa Zanzibar kuzingatia katiba na sharia kwa mjibu wa katiba.
Hata hivyo katika baadhi ya migogoro iliyosalia kutokana na uchaguzi mkuu waangalizi hawa wamewataka wanasiasa kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani badala yake wanapaswa kuwa kiungo mhimu katika suala zima la kudumisha Amani.BBC
Post a Comment