Viongozi
wa chama cha demokrasia na maendeleo mkoani Rukwa wameamua kuachia
ngazi kwa kujiuzuru, ambapo mwenyekiti wa chama hicho na katibu wa mkoa
huo pamoja na baraza zima la uongozi la mkoa wametangaza kuwa watabaki
kuwa wanachama wa kawaida, kwa kile walichokidai kutoridhishwa na
maamuzi ya makao makuu katika uteuzi wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu
kupitia chama hicho.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Sumbawanga mwenyekiti wa
Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Zeno Nkoswe, amesema licha ya kutoridhishwa
na uteuzi wa Aida Kenani kuwa mbunge wa viti maalumu kutoka mkoa huo wa
rukwa, pamoja na makao makuu ya chama kupewa taarifa mapema kuwa
kiongozi huyo hivi sasa amekuwa msaliti, kwani mara tu baada ya kura za
maoni amekuwa anakipigia debe chama cha TLP, lakini pia kutotekelezwa
kwa ahadi ya kuwalipa mawakala zaidi ya 1,000 waliosimamia uchaguzi
kwenye vituo mbalimbali, pia imekuwa sababu ya wao kujiuzuru nafasi zao.
Kwa upande wake katibu wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Ozem Chapita,
akitoa ufafanuzi wa hatua hiyo amesema uteuzi wa mtu ambaye anaonekana
ni msaliti, kunaweza kukaathiri hata uwezekano wa chama hicho
kilichoshinda viti kumi kati ya tisa vya udiwani, kuweza kuiendesha
halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kwa kuwa na meya wa manispaa, kwa
kushindwa kupata kura za kutosha.ITV
Post a Comment