Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama
hicho Bw Twaha Taslima wakati akitoa azimio la baraza baada ya
kumalizika kikao cha baraza kuu hapa Zanzibar ambapo amesema uamuzi wa
aina hiyo utaiweka Zanzibar katika wakati mgumu kiuchumi na kisiasa huku
akisisitiza haja ya zoezi la kura lirudi kama sheria inavyotamka.
Aidha kiongozi huyo wa juu wa CUF ambaye alimbatana na viongozi
wengine wa juu wa chama hicho kuzungumza na waandishi wa habari amesema
kuna athari kubwa za uchaguzi mkuu wa jamhuri ya muungano endapo
uchaguzi mkuu wa Zanzibar utafutwa kwa vile wapiga kura na daftari
lilotumika ndio hao ambao wanalaumiwa wana kasoro huku pia akisisitiza
maamuzi ya mwenyekiti wa tume amesababisha uvunjaji mkubwa wa katiba.
Zanzibar bado imeendelea kuwa na mvutano wa kisiasa ambapo wananchi
wa visiwa hivi bado wameendelea kuwa katikati baada ya kila upande
unaovutana kuwa na misimamo tofauti na serikali ya Zanzibar iliyoko hivi
sasa ikisitiza haja ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wote wa Zanzibar
unaowahusisha rais, wawakilishi na Madiwani.ITV
Post a Comment