BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI LILI;MALIZA MUDA WAKE [PICHA KUTOKA MAKTABA]
Makada wanne kutoka chama cha mapinduzi
wilayani Masasi wamejitosa katika
kinyang’anyiro cha kumpata mwenyekiti wa
halmashauri ya mji wa Masasi mkoani
Mtwara.
Katibu msaidizi wa chama hicho wilayani
humo Ajali Mpataga aliiambia Blog ya
Mtazamo Mpya leo kuwa waliochukua fomu
na kufanikiwa kuzirejesha ni pamoja na
diwani wa kata ya Mumbaka Nikwanya
H.Sadiki na Philemoni Millanzi diwani wa
kata ya Migongo.
Wengine ni aliyekuwa makamu mwenyekiti
katika baraza lililopita la madiwani la
halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa
kata ya Temeke Selemani Uledi Nivako
pamoja na diwani wa kata mpya ya Napupa
Sospeter Nachunga.
Mpataga alisema wagombea hao watapigiwa
kura na madiwani wenzao kutoka kwenye
Halamshauri hiyo yenye jumla ya madiwani
18 huku kati yao 14 ni wa kuchaguliwa na
wanne ni wale wa viti maalumu ambao wote
wameteuliwa kutoka chama cha mapinduzi.
Alisema uchaguzi huo utafanyika siku moja
kabla ya tarehe ya kuapishwa na kuanza
rasmi kwa baraza jipya la Madiwani ambapo
alisema kuwa hadi sasa bado wanasubiri
mwongozo ni lini madiwani hao wataapishwa
tayari kuanza kazi.
Katika hatua nyingine katibu huyo msaidizi
wa CCM wilaya ya Masasi Ajali Mpataga
aliiambia blog ya mtazamo mpya kuwa kwa
upande wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi
tayari wanachama wawili wamechukua fomu
kuomba nafasi ya kuwa mwenyekiti wa
halmashauri hiyo.
Aliwataja wanachama hao kuwa ni Juma
Satma aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la
madiwani lililopita ambaye pia ni diwani wa
kata ya Chiungutwa pamoja na diwani mpya
wa kata ya Mwena Nestory Chilumba.
Alisema wanatarajia kupata wenyeviti bora
na wazuri kutoka kwenye halmashauri zote
mbili zinazounda wilaya ya Masasi
watakaoendana na kasi ya Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania Dk.John
Magufuli.

Post a Comment