0
Mwenyekiti wa vyama vya ushirika wilayani
ya Masasi (AMCOSS) Selemani Ndege
akizungumza kwenye mahafali ya 24 ya chuo
cha maendeleo ya wananchi wilaya ya Masasi
siku ya ijumaa.

baadhi ya wahitimu walioshiki kwenye mahafali 
 wanachuo wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi

Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi ya Masasi Fred Mwakagenda akiongea kwenye mahafali hayo
mwanachuo akitunikiwa cheti cha kuhitimu chuo 

 Na Hamis Nasiri,Masasi.
WANAFUNZI wanaosoma katika chuo cha
maendeleo ya wananchi Masasi mkoani
Mtwara (FDC) hususani wasichana
wameaswa kutorubuniwa kimapenzi na
wananume kabla ya kuhitimu mafunzo yao
kwani kwa kufanya hivyo itawasababishia
washindwe kufikia malengo waliyojiwekea.
Ushauri huo ulitolewa jana wilayani humo na
mwenyekiti wa vyama vya
ushirika vya msingi (AMCOS) katika
halmashauri ya wilaya ya Masasi,
Selemani Ndege wakati alipokuwa
akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho
kwenye mahafali ya 24 ya kuhitimu masomo
yao kwa niaba ya mwenyekiti
wa chama kikuu cha ushirika mkoani Mtwara
MAMCU.
Aidha chama hicho kikuu cha MAMCU
kimetoa msaada wa shilingi Milioni tano
kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali
chuoni hapo ikiwemo ujenzi
wa mabweni.
Alisema kuwa wanafunzi wanaosoma katika
chuo hicho hasa wasichana
wasikubali kurubuniwa na wanaume
kujihusisha katika mahusiano ya
kimapenzi kwani wanaume ni waongo
wanapomuhitaji msichana kimapenzi.
Ndege alisema anatambua kuwa hadi
wanafunzi hao kuweza kuhitimu masomo
yao ya ufundi wa kushona nguo,utengenezaji
wa magari,ufundi
selemala,upishi,uash­i ufundi wa umeme wa
majumbani na umeme wa magari
ni wazi kuwa wamevuka vikwazo vingi hasa
kwa wasichana.
“Sisi wanaume tumeumbwa kuwa waongo
kwa nyinyi wasichana hivyo nawaasa
wasichana msikubali kurubuniwa na
wanaume someni ili muweze kutimiza
malengo yanu,”alisema Ndege
Akisoma taarifa fupi ya chuo mkuu wa hicho,
Fred Mwakagenda alisema
chuo hicho kipo chini ya wizara ya
maendeleo ya jamii jinsia na watoto
lakini kinakabiliwa na changamoto lukuki
ikiwemo ya ukosefu wa chumba
cha kusomea (maktaba).
Alisema changamoto zingine ni ukosefu wa
karakana kwa fani mbalimbali
na kusisitiza kuwa serikali ifanye kila hali
kwenda katika chuo ili
kujionea changamoto hizo ambazo
zinakwamisha utendaji wa kazi.
Mwakagenda aliongeza kuwa jumla ya 53
wanahitimu mafunzo yao ya miaka
miwili ambapo wanaume ni 45 na wasichana
nane wahitimu hao ni kati ya
wanachuo 81 ambao walianza chuo huku
chuo hicho kikiwa na jumla ya
wanachuo 188.
Alisema chuo cha maendeleo ya wananchi
Masasi kilijengwa mwaka 1963
kikiitwa chuo cha maendeleo ya vijijini chini
ya halmashauri ya Masasi
mwaka 1975 kilibadilishwa jina na kuitwa
chuo cha maendeleo ya
wananchi chini ya wizara ya elimu ya taifa
ambapo vilianzishwa baada
ya baba wa taifa hayati Mwalimu Julius
Nyerere kuiga vyuo vya ufundi
Sweeden Folk High School.
MKUU wa chuo cha maendeleo ya wananchi
wilaya ya Masasi Fred Mwakagenda
akizungumza wakati wa mahafali ya chuo
hicho.
Mgeni rasmi akioneshwa jiko linalotumia nishati ya jua akiwa na baahi ya walimu wa chuoni hapo

Post a Comment

 
Top