Matukio ya ajali za ndege yameendelea kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya habari duniani.
Ikiwa ni siku chache baada ya ndege
ya Urusi kuanguka na kuua zaidi ya watu 200 huko Sinai, Misri taarifa
nyingine iliyotufikia muda mfupi uliopita ni wa hii ajali nyingine
iliyotokea Sudan Kusini na kuua watu 41.
Ndege hiyo mali ya Serikali ya
Russia ambayo ni maalum kwa kubeba mizigo ilikua na abiria wachache huku
ikidaiwa kuangukia watu ardhini na kufanya idadi ya waliopoteza maisha
kufikia 41.
Ndege ilikuwa ikitokea uwanja wa ndege wa Juba kuelekea mji wa Paloch
katika jimbo la Upper Nile na ilianguka kwenye ukingo wa Mto Nile.Maafisa wa uwanja wa ndege wamesema mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo pamoja na mtoto mdogo ndio waliweza kunusurika.
Airplane just crashed near Juba Int’l Airport shortly after taking off. #EyeRadio’s D Santo: over 40 passengers died pic.twitter.com/SuFExWfX0Z
— Eye Radio Juba (@EyeRadioJuba) November 4, 2015
Post a Comment