Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza na
ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya
taifa ya Algferia kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa
kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe
la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.
Elius Maguli alianza kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 43
kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto
Hajji Mwinyi. Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao
1-0.
Algeria walisawazisha goli dakika chache baada ya kipindi cha pili
kuanza mfungaji akiwa ni Slimani Islam bao ambalo limefungwa kutokana na
uzembe wa walinzi wa Stars.
Dakika za mwanzo za kipindi cha pili Stara ilicheza mpira wa kasi na
kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 54 lililofungwa na Mbwana
Samatta baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Algeria kisha kufunga goli
kwa ustadi wa hali ya juu.
Muda mfupi baada ya Stars kupata goli la pili kocha alifanya
mabadiliko kwa kumpumzisha Elius Maguli na nafasi yake kuchukuliwa na
Mrisho Ngassa wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Muthir
Yahya.
Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria
Dakika ya 71 kipindi cha pili, Slimani Islam alifunga goli la kwanza
kabla ya kuisawazishia Aligeria dakika ya 74 goli lililotokana na
kutoelewana kwa safu ya ulinzi ya Stars na kutoa mwanya kwa Slimani
kuisawazishia timu yake. Kikosi cha Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe,
Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Himid Mao, Thomas Ulimwengu,
Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Elius Maguli na Farid Musa. Wlioanzia kwenye benchi: Ailishi Manula (GK) Salim Mbonde, Mohamed Hussein, Simon Msuva, John Bocco, Mrisho Ngassa na Malimi Busungu.
Post a Comment