0


           Nilihisi kama nipo ndani ya ndoto vile, katika jioni ile, haki ilikuwa ni ndoto ambayo ilikuwa imekuja bila ya kuyafunga macho yangu labda kuwemo kwenye usingizi.
Uzuri wa yule msichana hakika uliendana vyema na sauti iliyokuwa ikimtoka kinywani mwake. 
Mungu alimpa kila kitu si sauti tu sura nzuri, umbo zuri la wastani , huku mashavu yake yakipambwa na vishimo viwili , kimoja upande wa kulia wa shavu lake na kingine upande wa kushoto wa shavu lake. Zilipamba vyema urembo wa msichana yule, na kuleta utofauti na wanadamu wengine, hakika Mungu alimuumba katika utulivu wa hali ya juu utulivu ulisabaisha kuleta burudani kwenye mboni za macho yangu punde nilipoigeuza shingo yangu kufatisha sehemu ilipokuwa ikitoka sauti ile ya mwanadamu yule.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kumjua msichana aliyekuwa akiitwa Irene ndani ya ubongo wangu.
Mwanzoni si kuwa nalijua jina ilo kabisa, kutokana nilivutiwa naye nilifanya juu chini kufatiria habari zake. Na baada ya purukushani katika siku mbili tatu hatimaye niliweza kulifahamu vyema jina hilo, pamoja na baadhi ya vitu ambavyo nilikuwa niliviona vya msingi katika kukamlisha hadhima yangu juu ya msichana yule.
Sikupata shida sana kutokana na umarufu wangu, na watu kunithamini sana, na hadhi niliyokuwa nayo ndani ya chuo. Vyote hivyo vilitokana na uwezo wangu wakukimbia katika mbio fupi kuliko mtu mwingine chuoni pale katika mashindano mbalimbali.
Ulikuwa kivutio kikubwa sikuwahi kuwa na mpinzani kabisa. Ilo lilinijengea jina kwa kiasi kwamba ilinifanya niwe rahisi kupata habari zake.  Kwasababu rafiki zake walinitambua vyema, sikupata tabu hata pale nilipoenda kuzungumza nawo kwa lengo la kutaka kujua habari zake walinipa ushirikiano mkubwa sana.
Muda mchache niliweza kumfahamu vyema ndipo malindo yangu  yalipoanza, na hatimaye Irene aliingia kwenye himaya yangu.
                                             *********
Mambo yote yaliyo tokea kipindi cha nyuma kidogo yalinifanya wazo la Irene kututoka kichwani mwangu, siku hadi siku kuwa gumu zaidi. Wakati huo afya yangu ilikuwa imelejea kama zamani, licha ya daktari kusisitiza nisifikirie chochote kile haswa kitu kiitwacho mapenzi kwa kipindi chote nikiwa bado najiuguza kabla sijaenda India aliposhauri juu ya uchunguzi zaidi kuhusu moyo wangu.

Penzi lake kwangu lilikuwa kama vile penzi la kipofu, nilipagawa sana na msichana yule, sidhani kama ulikuwa upendo wa kawaida, nilihisi uwepo wa nguvu za giza katika jambo lile. Lakini fikra zangu hazikuwa zikikubali moja kwa moja, hata kunakipindi nilijilaumu sana lakini mwishowe nilijikuta nikijipuuza mwenye na Irene akirudi tena ndani yangu. Na kujipongeza ya kuwa nilikuwa na mapenzi ya dhati na binti huyo , licha ya kutoonesha kunithamini kipindi chote nilichokuwa nikiugua niliamini ipo siku ningeweza kumweka sawa na kurudi katika upande wangu. Juu ya kuwa anipendi suala hilo halikuwa likipata nafasi kwangu.
Nikikumbuka maneno yake, hata nguvu zilikuwa zikiniishia.
Kuna baadhi ya siku macho yangu yalikuwa ya kivimba na kuwa mekundu kutona na kilio ambacho hakikuwa na mbembelezaji. 
Nilikuwa nikishikwa na uchungu sana kila nikimfikiria msichana yule hata ilifika kipindi mama yangu alikuwa anapoteza furaha baada ya kubaini hali yangu. Mama hakuwa akifurahishwa na hali ile ilikuwa ikijitokeza upande wangu lakini hakuwa namna.
                                   **********
Zilipita wiki tano baada ya kupona majeraha yote, grafla hali yangu ilianza kubadilika mwili ulianza kukosa nguvu na maumivu madogo yalianza kujitokeza eneo la kushoto la kifua changu ambapo ulipo wangu moyo. Hali yangu ya kimwili kijumla ilianza kudhoofu tofauti na mwanzoni.
 
Nilimueleza mama jinsi nilivyokuwa najisikia na hata hali yangu ilivyokuwa ikibadilika, kumbe hata yeye aliiyona.

Maskini mama alianza kutafuta pesa kwajili ya kutibiwa na kibaya zaidi haikuwa hapa nchini, bali nje ya nchi kutokana hali ile ambayo daktari alishaiyona kabla na alishasema nini cha kufanya mapema.
Mama aliangaika pekee yake sehemu mbali mbali hadi kule mzee alipokuwa akifanyia kazi ila bado hakufanikiwa kupata pesa ya kutosha, angalau walimpa pesa kidogo lakini zilikuwa hazitoshi kugharamia safari ile pamoja na matibabu ndani ya nchi ya India.
Ilimbidi Mama auze moja ya nyumba yetu ilitoachia marehemu baba, aliuza tu ilimladi iliaweze kufanikisha matibabu yangu yalikuwa yanaitajika kwa namna yoyote ile, maana mambo yalionekana yangeweza kuwa mabaya kadri siku zilivyokuwa zinaenda.
Mipango ya safari ilipangwa haraka baina yangu na mama ambaye ndio alikuwa akinisimamia mwanzo hadi mwisho katika ugonjwa wangu.
Na tulipo hakikisha mipango imekaa sawa mama alimchukua mdogo wangu Criss na kumpeleka kwa mjomba iliakakae kipindi chote ambacho tutapokuwa india. Tungeweza kwenda naye licha umri wake kuwa mdogo lakini ilitubidi kwasababu ya pesa kuwa haitoshi ilitulazimu. Sikupenda hata kidogo litokee lile kwasababu upendo wangu dhidi ya mdogo wangu. Macho yangu hayakuwa tayari kuipoteza taswira yake ijapokuwa ni kwa muda mfupi ila kitendo kile kiliniuma sana.
                                                        **********
Maneno yale yalikuwa yameandikwa na kaka Eddy, ndani ya kijitabu kile yaliniingia kisawasawa kwa mara nyingine. Moyoni mwangu nilizidi kupata hasira juu ya viumbe viitwavyo wanawake moja kwa moja nilijua tu uwenda Irene ndio chanzo cha ugonjwa ule wa kaka na safari ya kuelekea huku India. Katika mwanzo ule ambao mpaka leo umebaki kuwa historia isiyofutika kichwani mwagu, huku ikiendelea kunisurubu na kuniachia maumivu makali katika kila pembe ya mwili wangu.
Gafla mazunguzo yale ya mjomba na mama ambayo yalikuwa ndio kwanza mabichi yakapita kichwani mwangu nikaanza kujiuliza lakini kwanini naye mjomba ajilize kama mtoto kisa mwanamke, amemkosea nini mjomba?, maswali yalinikaba koo, majibu hayakuwa karibu ubongo wangu ulionekana nao kunisaliti, katika usaliti wa aina yake.

Post a Comment

 
Top