Msingi mkuu wa kufahamu lugha ni kujua jinsi sentensi zinavyoundwa kwakuwa sentensi ndio haswa tunazotumia katika mazungumzo na kuandika. Sentensi ni kikundi cha maneno chenye kubeba maana fulani. Mfano wa sentensi ni :
Unaitwa nani : What is your name
Wao hawakuwepo hapa. – They were not here
John ni muandishi wa Mbuke Times. John is the author of Mbuke Times.
Ni kweli kuwa kujua msamiati ni jambo la msingi katika kuiweza lugha, hata hivyo kujua msamiati bila kuzingatia kanuni na muundo wa lugha husika ni kazi bure. Angalia mfano wa sentensi hizi za Kiswahili ambazo zinatumia maneno sahihi kabisa ila muundo mbovu, utaelewa nini ninasema.
Jana wao kwetu wanakuja.
John muandishi Mbuke ni .
Jambo la kwanza: Fahamu aina za mionekano ya sentensi..
Aina za mionekano ya sentensi
1..Muonekano wa kukubali au tuseme kueleza jambo kwa hali chanya:
Mfano : John is eating ( John anakula).
We like Mbuke Times ( Tunaipenda Mbuke Times)
2. Muonekano wa kukataa jambo au kuelezea kwa hali hasi
Mfano: John is not eating rice ( John hali wali)
She does not like Mbuke Times ( Yeye hapendi Mbuke Times).
3. Muonekano wa kuuliza
Is John eating ugali ? (Je, John anakula ugali?)
Does she like Mbuke Times ? (Je, anaipenda Mbuke Times ?)
Don’t you know that ? ( Je, haufahamu hilo ?)
Jambo la pili: Nyakati
Jambo lingine la msingi kuzingatia ni kufahamu kuwa sentensi yoyote katika muonekano wowote kati ya hiyo iliyotajwa hapo juu, huwa inaangukia kwenye nyakati fulani, na kwamba kila nyakati inabadilisha jinsi muundo wa muonekano wa sentensi.
Mfano:
A. Wakati uliopo hali ya kuendelea(Present Continous Tense)
Muundo wa kukubali : John is eating. (John anakula)
Muundo wa swali: Is John eating ? .(Je John anakula?). Are they coming ? ( Je, wanakuja?)
Muundo wa kukanusha: John is not eating ( John hali )
B: Wakati uliopita wa kawaida ( Simple Past Tense)
Muundo wa kukubali: John ate. (John alikula)
Muundo wa swali: Did John eat ? ( Je, John alikula ?)
Muundo wa kukanusha: John did not eat (John hakula)
C: Wakati wa Uliopo hali ya kawaida (Simple Present Tense)
Muundo wa kukubali: John eats. ( John hula)
Muundo wa swali: Does John eat ? ( Je, John hula ?)
Muundo wa kukanusha: John does not eat. ( John huwa hali)
Zipo nyakati nyingine nyingi, utajifunza zaidi kuhusu nyakati katika somo lake maalum.
ZINGATIA: Kumbuka somo hili kwani tutakapoanza kuchambua Nyakati Mbalimbali itakupasa ujue kuwa kuna aina tofauti za mionekano na kwamba kuna kanuni maalum ya kuandika sentensi katika mionekano hiyo katika kila nyakati.
Kama ulivyoona hapo juu, mifano A mpaka C, kuwa tunaanza na maneno tofauti kwa kila aina ya nyakati. Mfano Wakati Uliopo hali ya kuendelea tunaanza na IS au ARE, bali kwa Wakati Uliopita Hali ya Kawaida(Simple Past) tunaanza na neno DID
Post a Comment