Na.Ahmad Mmow. Lindi
Baraza la ushauri la CHADEMA mkoa wa Lindi lilofanya kikao chake kijijini Mtama wiki iliyopita limemkaimisha Selemani Methew Lowongo, kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa Lindi.
Baraza la ushauri la CHADEMA mkoa wa Lindi lilofanya kikao chake kijijini Mtama wiki iliyopita limemkaimisha Selemani Methew Lowongo, kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa Lindi.
Selemani Methew Lowongo (Kushoto) Akipokea Kadi ya Uanachama alipojiunga na Chama cha Chadema.
Lowongo
mchezaji wazamani wa timu za Simba na Yanga, ambaye aligombea ubunge
katika jimbo la Mtama katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita,
alipitishwa na baraza hilo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa
mwenyekiti wa chama wa mkoa, Ally Chitanda aliyejiunga na CCM.
Katibu
wa CHADEMA mkoa wa Lindi, Mohamed Mahadhi alithibitisha kuwa Lowongo
alikaimishwa mwanzoni mwa wiki hii na wajumbe 59 waliohudhuria baraza
hilo kutoka wilaya za Ruangwa, Kilwa, Nachingwea, Lindi na Kilwa.
Alisema baada ya kuondoka Chitanda ambaye sasa nidiwani wa kata ya Nangowe wilayani Nachingwea, nafasi hiyo ilikuwa wazi.
"Baada
ya Chitanda kukihama chama na kujiunga na CCM nafasi hiyo ilikuwa wazi.
Baraza liliona ana uwezo wa kukiongoza, kukijenga na kukieneza chama"
Baraza limeona anaimudu nafasi hiyo na atakaimu hadi utakapofanyika
uchaguzi," alisema Mohamed.
Alisema
kikao hicho ambacho kilikuwa cha kufanya tathimini ya uchaguzi uliopita
kilibaini sababu mbalimbali zilizosababisha kutofanya vizuri kwenye
uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita. Alizitaja sababu hizo kuwa ni
viongozi wa kanda, wilaya na mkoa kutokwenda vijijini mara kwa mara.
Sababu
nyingine iliyotajwa na katibu huyo ni tangazo la kuachiana maeneo kwa
wagombea wa vyama vilivyounda UKAWA kuchelewa. Alibainisha kuwa tangazo
hilo lilitolewa wakati wagombea wa vyama hivyo walishafanya maandalizi
na kutumia gharama zao.
Hivyo
ilikuwa vigumu wagombea hao kuachiana, na kusabisha CCM kushinda nafasi
za ubunge na udiwani katika baadhi ya maeneo. Vilevile katibu huyo
alisema kikao hicho pia kilibaini chama hicho kimeenea katika mkoa huu.
Kwa
madai kwamba kimeweza kupata madaiwani kwenye baadhi ya kata. Huku
akitoa pongezi kwa makao makuu ya chama hicho kwa kumteua Latifa Chande,
ambaye anatokea mkoa huu, kuwa mbunge wa viti maalum.
Kwenye
uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita, Luwongo alishindwa kwa takribani
kura 13000 alizopata dhidi ya mbunge mteule wa jimbo hilo, Nape
Nnauye(CCM) aliyepata kura takribani 18000. Ambapo Isihaka Mchinjita wa
CUF alipata kura 10000.
Post a Comment