Kundi la
wapiganaji la Islamic State limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya
mashambulio ya mjini Paris Ijumaa usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais
Hollande ameelezea mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa
na IS ambao alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi.
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume
wanane waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo
katika sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.
Wakuu wanasema paspoti ya Syria ilionekana karibu na mwili moja.
Watu kama 80 walikufa katika tamasha la muziki wa roki - ambako washambuliaji waliwakabili mateka wao na kuwapiga risasi.
Hapo awali, watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi nyingi dhidi ya mikahawa iliyo karibu na kusababisha hasara kubwa.
Wengine waliripua mabomu karibu na uwanja wa michezo wa taifa, ambako Ufaransa ikicheza mechi ya kandanda na Ujerumani.
|
Post a Comment