Wapiganaji wa islamic state
Kundi la kigaidi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi la Paris.
Katika
taarifa yake iliochapishwa mtandaoni,kundi hilo la kijihadi ,limesema
kuwa shambulizi hilo lililenga kuielezea Ufaransa kwamba pia nayo ni
miongoni mwa mataifa yanayolengwa na kundi hilo.Kundi hilo limesema kuwa lilichunguza maeneo yalioshambuliwa na kutekeleza mashambulizi hayo kwa kuwatumia ndugu wanane waliovalia mikanda ya vilipuzi mbali na kujihami na bunduki.
Taarifa hiyo inadai kwamba ndugu wanne waliovalia vilipuzi na kujihami na bunduki waliyalenga maeneo yaliotengwa katikati mwa mji wa Ufaransa.
Taarifa hiyo pia imeendelea na kutaja mji wa Paris kama mji mkuu wa 'uchafu na upotoshaji'.
Post a Comment