0
 


Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi wakitia saini mkataba wa ruzuku kwa ajili ya kufanikisha programu za UN Tanzania, uliofanyika ofisi za EU Dar es Salaam jana. (Picha na UN).


JUMUIYA ya Ulaya (EU) imetia saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN) wa ruzuku ya Euro 200,000 (takribani Sh 478,000,000) kwa ajili ya shughuli za maendeleo zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania.

JUMUIYA ya Ulaya (EU) imetia saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN) wa ruzuku ya Euro 200,000 (takribani Sh 478,000,000) kwa ajili ya shughuli za maendeleo zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania.
Shughuli hiyo ya utiaji saini ilifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi. Utiaji saini huo ulifanyika Ofisi za EU jijini Dar es Salaam jana na kushuhudiwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Jumuiya ya Ulaya.
Ruzuku hiyo kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa imelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU na UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi. Maeneo hayo ni muhimu kwa shughuli za EU na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Akisisitiza mchango wake kwa One UN, Balozi wa EU, Filiberto Ceriani Sebregondi alisema kwamba Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyoweza kufanya kazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu wa nchi hii.
EU nchini imekuwa na ushirikiano katika programu kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, hasa IOM, UNICEF, UNDP, UNODC, UNHCR, FAO, UNESCO, IFAD, UN Women na WFP. Kwa sasa EU imeshatoa euro milioni 43 kwa ajili ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.

Post a Comment

 
Top