0
News
Taarifa iliyoripotiwa  muda mfupi uliopita na kuthibitishwa na Serikali inahusu Msiba wa Waziri huyo, Abdallah Omar Kigoda ambaye alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Kigoda rip
Hiyo ni taarifa kutoka Ofisi ya Bunge ikionesha Waziri huyo amefariki leo Jioni katika Hospitali ya Appolo ambako alikuwa akitibiwa.. Serikali iko kwenye Mipango ya taratibu za kusafirisha Mwili wa Marehemu pamoja na Mazishi kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu.
Kigodz & JP
RIP Dk. Kigoda… Hapa alikuwa na Mgombea Urais wa TZ kupitia CCM, Dk. John Magufuli.
Assah
Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
Serikali inasikitika kutangaza kifo cha Dk. Abdallah Kigoda aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kilichotokea Hospitali ya Appolo India leo.. Taarifa kuhusu kusafirisha mwili wa Marehemu na Mazishi mtaendelea kupatiwa. Dk Kigoda alilazwa tarehe 18 September 2015 ambako alikuwa akipatiwa matibabu” >>> Assa Mwambene,

Post a Comment

 
Top