Hatimaye lile tukio la utolewaji wa Tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) ambazo
hutolewa kila mwaka kwa wanamichezo wanaofanya vizuri, zimekamilika
usiku wa October 12 kwa wanamichezo, taasisi na viongozi waliofanya
vizuri katika kipindi cha miaka 10, Tuzo hizo safari hii zimekuwa
tofauti na miaka yote kwani waliopewa Tuzo ni wale waliofanya vizuri
katika kipindi cha miaka kumi.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa maalumu mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga Rais Kikwete
kwa kumaliza muda wake madarakani na kuheshimu mchango wake katika
kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala wake. Ikumbukwe kuwa
Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi iliyochangia
kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
Tuzo zimetolewa kwa wanamichezo
waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi, viongozi waliochangia
kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na Tuzo ya heshima
kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis Cheka, Mbwana Samatta, Iddi Kipingu, Abdallah Majura na Hashim Thabiti
Kanali Iddi Kipingu akipokea Tuzo yake ya heshima kwa kusaidia kuinua michezo kwa muda mrefu toka yupo shule ya Makongo
Abdallah Majura akikabidhiwa Tuzo ya heshima katika kuinua michezo sasa kafungua kituo cha Radio kinachojihusisha na michezo.
Mwenyekiti
wa TASWA Juma Pinto akimkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya heshima akiwa
pamoja na mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Meki Sadiki, waziri wa michezo Dk
Fenella Mukangara na Dioniz Malinzi.
Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub akikabidhi jezi ya Taifa Stars kwa Rais Kikwete ikiwa imesainiwa na wachezaji wote.
Post a Comment