Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa
katika viwanja mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa huku
kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu muhimu.
Uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha Coastal Union
kutoka jijini Tanga, mchezo utakaoanza majira ya saa 10:30 jioni, huku
Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United uwanja wa Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara.
Wachimba
Almasi wa Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga, Toto African watakuwa wenyeji wa maafande wa Mgambo
Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakata
miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika
uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, huku watoza ushuru wa jiji la
Mbeya katika uwanja wa Sokoine Mbeya City wakiwa wenyeji wa Majimaji
kutoka mkoani Ruvuma.
Ligi
hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo miwili kuchezwa, Tanzania
Prisons watakuwa wenyeji wa African Sports katika uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya, JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa
Karume jijini Dar es salaam.
Post a Comment