MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KOZI YA
MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII
- Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba
kujiunga na kozi ya Muhudumu wa afya ngazi ya jamii (Community Health)
kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali
umefanyika na waombaji 3985 kati ya 9797 wameteuliwa kujiunga na vyuo
mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi
(Profiles) za waombaji
- Waombaji
wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa
wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni
Ijumaa tarehe 04 November 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi
hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa au ingia katika ukurasa wako binafsi (Profile) kudhibitisha.
- Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 05 November 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo katika nafasi 278 zilizobaki wazi.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
28 October 2015
Post a Comment