Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho,
amejitetea kuwa kinachodhaniwa ni lugha mbovu aliyotumia baada ya
kushindwa na Southampton ni kwa kuwa Kiingereza si lugha yake ya mama.
Mourinho
alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya Pauni za Uingereza 50,000 na
shirikisho la Kandanda la Uingereza. Alidai kuwa maafisa wa kandanda
nchini humo wanaogopa kuipa timu yake penalti inayostahili. Madai ya
Morinho yalitolewa baada ya tume huru maalimu kutoa sababu za adhabu
hiyo kutolewa na FA. Kocha huyo machachari wa Chelsea hakuhudhuria
kilichomwadhibu lakini alituma taarifa ya maandishi kujitetea. Alikiri
kuwa alikosa adabu lakini akakanusha kuwa alitilia shaka hadhi ya refa
Robert Madley. Huku akijitetea, Moorinho alisema kuwa makosa yaliyompata
ni sawa na yale yaliyowahusu makocha wengine watano wa Premier League.
Mbali na kukosoa kiwango cha faini aliyotozwa, Mourinho pia alisema kuwa
kupigwa marufuku uwanjani kwa mechi moja, ambako kumeahirishwa
kutekelezwa kwa mwaka mmoja, "kulimshangaza". Wenger hakuchukuliwa hatua
yo yote alipomsukuma Mourinho katika eneo la wakufunzi katika Stamford
Bridge Oktoba mwaka 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment