0
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza leo mbele ya waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam.
Amesema kutokana na matukio yaliyotokea katika kumpata mgombea Urais kupitia chama chake ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo ameamua kuondoka ndani ya chama hicho na sasa yupo huru.
Kingune amesema hawezi kuhimili chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee na makada wengine.
Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki zake za kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi yake..”Hali ya sasa jinsi ninavyoona vijana, wafanyakazi, wakulima wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa mabadiliko kwa sababu wakati tukiwa TANU tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”KINGUNGE

Post a Comment

 
Top