0
MTENJELE CUP 2015
Group A
Manyan`gunyan`gu fc 3 Vs  0 Ngarinje fc
Mechi za ufunguzi wa kombe la Mtenjele cup 2015 ilianza kutimu vumbi leo katika uwanja wa Bomani  zilizokutana timu ya Manyan`gunyan`gu fc Vs   Ngarinje fc ambapo kila timu kipindi cha kwanza zilianza kwa mbwembwe ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya Manyan`gunyan`gu fc iliongoza kwa goli moja.
Katika kipindi cha pili mpira ulichezwa kwa rafu za aina yake timu ya Ngarinje fc iliposaka angalau goli la kufutia machozi wakiogopa kuchekwa lakini walikomaliwa na waongezwa goli mbili mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha kumaliza mpira matokeo yalikuwa Manyan`gunyan`gu fc ,3 Vs  0 Ngarinje fc.
Kesho kutakuwa na mchezo mwingine wa group B zitakachochezwa hapa hapa mjini Masasi mkoani Mtwara.

Post a Comment

 
Top