Waendesha mashitaka mwishoni mwa mwaka 2013 waliitaka mahakama hiyo ya ICC kutoa uamuzi kwamba Kenya ilishindwa kuchukua hatua kuhusu ombi la upande wa mashitaka kukabidhiwa data za kifedha za Kenyatta, taarifa za simu pamoja na nyaraka nyingine wanazosema zingeweza kuthibitisha kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu anaohusishwa nao.
Waendesha mashitaka pia wametaka mahakama ya ICC kupeleka suala hilo katika chombo kijulikanacho kama baraza la makundi ya kitaifa, chombo chenye wajumbe kutoka mataifa 123 na linaloweza kutafakari kuchukua hatua.
Kesi dhidi ya Kenyatta ilivunjika mwishoni mwa mwaka jana baada ya mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda kuondoa shutuma dhidi yake za kupanga njama za ghasia baada ya uchaguzi mwaka 2007-08 ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuwawa.
Post a Comment