0








Wabunge  wa  Ujerumani  wamepiga  kura  kuunga  mkono mpango  wa  tatu  wa  uokozi  wa  uchumi  wa  Ugiriki  leo, licha  ya  idadi  kubwa  ya  wabunge  walioasi  miongoni mwa  chama  cha  kansela  Angela  Merkel, hali inayoashiria  kwamba  atapata  taabu  wakati  atakaporejea bungeni  kuomba  msaada  zaidi  kwa  Uturuki.
Wakikubali wito  wa  waziri  wa  fedha  Wolfgang Schaeuble  kuipa Ugiriki nafasi  ya  kuanza kujijenga upya, wabunge  wa  chama  cha  kihafidhina  cha  CDU waliasi kwa  idadi  ndogo  kuliko  baadhi   ya  wanachama   wa chama  hicho walivyotabiri.
Mpango  huo  ulipitishwa  bungeni  kwa  msaada  wa chama  cha  Social Democratic, chama  mshirika  katika serikali  ya  kansela  Angela  Merkel pamoja  na  chama cha  walinzi  wa  mazingira , The Greens, kwa  kura  454, dhidi  ya  113, na  wabunge 18  hawakupiga  kura.

Post a Comment

 
Top