0

Manchester United imeanza vizuri
mchezo wa kwanza wa mchujo
kuwania nafasi kuingia hatua ya
makundi ya michunao ya klabu
bingwa barani ulaya,
Baada ya kupata ushindi wa 3-1
dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji .
Brugge ilipata bao lao mapema
dakika ya 8 ya mchezo baada ya
kiungo wa Man U Michael Carrick
kujifunga.
Mshambuliaji mpya wa kikosi
hicho cha mashetani wekundu
Memphis Depay akasawazisha
bao hilo dakika ya 14 kabla ya
kuongeza bao la pili dakika 43,
kiungo aliyeingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Wayne
Rooney, Mbelgiji
Marouane Fellaini, akifunga bao la
tatu lilihitimisha ushindi huo.
Matokeo mengine ya michezo ya
mchujo kuwania kuingia hatua ya
makundi ya klabu bingwa ulaya
ni:
Astana 1 APOEL Nicosia 0

BATE Borisov 1 Partizan Belgrade
0
Lazio 1 Bayer Leverkusen 0

Sporting CP 2 CSKA Moscow 1

Post a Comment

 
Top