Watu watatu wamekufa na
wengine thelathini wamelazwa
hospitalini kutokana na mlipuko
wa ugonjwa wa kipindupindu
nchini Tanzania na hasa katika
mji wa kibiashara wa Dar es
salaam.
Wataalamu wa afya wamesema
kwamba mlipuko huo unapatikana
kwenye maeneo ambayo hayana
usafi wa kutosha na vyoo vya
kisasa hasa katika maeneo yenye
msongamano wa makazi katika
jiji hilo.
Maafisa wa afya tayari
wameshachukua hatua ili kuzuia
mlipuko huo usienee zaidi tangu
mlipuko mkubwa wa kwanza
ulioripotiwa kulikumba jiji hilo
mwaka 2009.
Wodi tengefu kwa wagonjwa wa
ugonjwa huo imeshaandaliwa
katika hospitali za wilaya ya
Kinondoni eneo ambalo
limeathiriwa vibaya na ugonjwa
huo.
Umma wa watanzania
wametakiwa kuwa waangalifu
baada ya kifo cha mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka
ishirini na saba,mwishoni mwa
wiki iliyopita baada ya kuonesha
dalili zinazoshabihiana na
magonjwa ya milipuko.
Dar es salaam ni mmoja kati ya
miji yenye idadi kubwa ya watu,
mji huo pekee una idadi ya watu
zaidi ya milioni tano.
Watu waishio katika makazi
holela wako katika hatari kubwa
ya kuambukizwa ugonjwa wa
kipindupindu kutokana na
kutokuwa na vyoo bora na vya
kisasa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment