0
Mlinda mlango wa Arsenal Petr
Cech aliokoa mara mbili mipira ya
hatari iliyokuwa ikielekea langoni
mwake na kuisaidia timu yake
kupata alama moja katika mechi
ya Ligi Kuu ya England dhidi ya
Liverpool.
Katika mchezo huo mikwaju
miwili ya Philippe Coutinho
ililenga mwamba huku kiungo wa
Arsenal Aaron Ramsey akikataliwa
goli alilofunga kipindi cha kwanza
kutokana na kuwa katika mstari
wa kuotea.
Cech aliokoa kwa mara nyingine
mkwaju wa karibu wa Christian
Benteke na kuucheza tena kwa
umahiri mpira uliopigwa na
Coutinho uliokuwa unaelekea
kwenye nyavu.
Juhudi za Alexis Sanchez ziliishia
kulenga mwamba kabla ya mlinda
mlango wa Liverpool Simon
Mignolet kuokoa mkwaju wa
Olivier Giroud.
Christian Benteke mwenye jezi
nyeusi akijaribu kufunga goli bila
mafanikio

Post a Comment

 
Top