Suruali ndefu zinazobana zina madhara
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 35
alilazimika kutolewa ndani ya suruali ndefu
aina ya Jeans, baada ya miguu yake kuvimba
kupita kiasi.
Hayo ni kwa mjibu wa jarida la Neurology,
ambalo huandika habari kuhusu upasuaji.
Alichuchumaa kwa muda mrefu sana ili
kuondoa bidhaa ndani ya kabati alipokuwa
akijiandaa kuhama nchini Australia.
Ilipofika jioni, miguu yake ilikuwa imekufa
ganzi na akashindwa kutembea.
Madaktari waanamini kuwa mwanamke huyo
alipatwa na maradhi yanayojulikana kama
compartment syndrome, ambayo
yalisababishwa na suruali yake ndefu yenye
kubana mno.
Ugonjwa huo ni mbaya sana na husababishwa
na kujuja kwa damu na kuvimba kwa misuli.
Tatizo hilo lilimfanya mwanamke huyo
kuteguka na kuanguka na akashindwa
kuinuka. Alisalia ardhini kwa saa kadhaa.
Alipofikishwa katika Hospitali ya Royal
Adelaide, sehemu ya chini ya miguu yake
ilikuwa na uvimbe m'baya.
Ingawa miguu yake ilikuwa na joto na damu
ilikuwa ikisambazwa vyema, misuli yake
ilikuwa haina nguvu na ilikuwa imeshapoteza
hisia.
Madaktari wengine wamesema kuwa
wamepokea visa kadhaa ambapo wagonjwa
wamelalamikia kudungwa dungwa pamoja na
kuganda kwa mapaja, baada ya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment