0

Chama tawala nchini Ethiopia cha Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front cha waziri mkuu Halemariam Desalegn, kimeshinda ushindi wa kishindo wa idadi yote ya viti vya bunge 546 kufuatia uchaguzi uliofanywa mwezi uliopita. Taarifa hii ni kulingana na mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi. Ingawa upinzani umedai kuwa serikali ilitumia mikakati ya mabavu kuhakikisha ushindi unakuwa wao. Aidha wasimamizi wa uchaguzi huo wa Umoja wa Afrika, wamesema uchaguzi ulikwenda vizuri bila ya kutokea matatizo yoyote. Huku kiongozi wa chama cha upinzani cha Blue Party, Yilkal Getnet, amepinga kabisa matokeo hayo na kusema Ethiopia hakuna uhuru wa kisiasa. Na kwamba chama tawala hakina kweli nia ya kuimarisha mfumo wa kisiasa wa vyama vingi.

Post a Comment

 
Top