BY-ZULFA MUSA NA BERTHA ISMAIL
Lema, wenzake 24 rumande kwa
saa nne
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na
watu wengine 24 juzi walijikuta wakiwekwa
mikononi mwa
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Arusha . Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema na watu wengine 24 juzi walijikuta
wakiwekwa mikononi mwa polisi kwa saa
nne kutokana na purukushani za
uandikishaji wa wapigakura katika mfumo
wa BVR.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni kwenye kituo
cha uandikishaji kituo cha Osunyai, Kata ya
Sombetini ambako watu hao akiwamo
mbunge walitiwa mbaroni.
Diwani wa Kata ya Sombetini, Ally
Bananga alisema mbunge huyo na watu
wengine walikamatwa huku wengine 13
wakijeruhiwa katika tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas alisema juzi kuwa tukio
hilo alikuwa amelisikia juujuu lakini
hakuwa amepata taarifa zaidi.
Mmoja wa washuhuda wa tukio hilo, Amiri
Ally alisema juzi saa 12.20 jioni Lema
alifika katika kituo hicho na kuuliza
kinachoendelea na kuhamasisha
waandikishaji kufanya haraka katika
kuandikisha lakini walitokea vijana kadhaa
waliodhaniwa ni wanachama wa CCM na
kuanza kumzuia mbunge huyo asiingie
ndani.
“Kila jioni Lema huwa anazungukia vituo
kuangalia maendeleo lakini hakuna jambo
linalotokea ila leo (juzi) kuna vijana ambao
huwa tunawaona kwenye misafara ya CCM
kama walinzi, walianza kumzuia Lema
asiingie ndani, walianza kusukumana na
wananchi nao waliingilia kati, ndio vurugu
zikaanza,” alisema.
“Vurugu zilipopamba moto polisi walikuja
na kuwakamata baadhi ya watu na
kuondoka nao akiwamo Lema na watu
wengine wakaanza kukimbia ovyo,”
alisema Amiri.
Mmoja wa watu waliojeruhiwa, Abduli
Adam alisema baada ya kuona mbunge
anasukumwa hovyo na vijana
walioonekana kama ni kutoka kwa walinzi
wa CCM aliingilia kati kutaka kumsaidia
lakini alichomwa kisu cha kichwa na
kuvuja damu nyingi.
“Mimi nilikuwa kwenye foleni nikashangaa
kelele upande wa pili kuangalia nikamuona
Mbunge Lema katikati, hivyo nikajitosa
kumsaidia nikachomwa kisu cha kichwa
sijui aliyenichoma na sasa niko njiani
naelekea hospitali ya Mkoa Mount Meru
kutibiwa,” alisema.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na
mwanasheria wa Chadema, mwenyekiti wa
Mtaa wa Osunyai, viongozi mbalimbali wa
chama na wananchi waliokuwa
wanajiandikisha kituoni hapo.
Kukamatwa kwa watu hao kulisababisha
shughuli ya uandikishaji kusitishwa
kutokana na vurugu kuzuka kwenye kituo
hicho saa 12 jioni badala ya saa 2:00 usiku
kama ilivyopangwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Akizungumzia tukio hilo, Lema alisema,
“Nimeshindwa kuelewa kukamatwa kwangu
baada ya kutoa taarifa polisi, inawezekana
vipi mlalamikaji akakamatwa na wahalifu
wakawa huru.”
Lema alisema kuanzia juzi alikuwa
anafuatiliwa na gari lililokuwa
linabadilisha namba za gari wakati
akitembelea vituo, baada ya kuona hali
hiyo alitoa taarifa polisi kuomba ulinzi.
Hata hivyo, alisema pamoja na kutoa
taarifa hakuna lolote lililofanyika.
“Mimi ni mbunge na nina wajibu wa kujua
kila linaloendelea katika zoezi hili,
nimekuwa ninafuatilia vituo kujua
nitasaidia vipi na nisingefanya hivyo,
mashine hizi zingepatikanaje, wanaosema
navunja amani si kweli,” alisema Lema.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Lema alisema yeye
ndiyo aliyewaita polisi ili kumsaidia ulinzi
baada ya kubaini kikundi cha vijana wa
CCM wakizuia watu kujiandikisha na
kumshambulia kwa mawe.
“Lakini mimi baada ya kupiga simu polisi
kuomba msaada polisi walifika kwa
haraka, lakini badala ya kukamata vijana
hao ambao walikuwa wakizuia watu
kujipanga mstari wakanikamata mimi na
wafuasi wangu 24 na kutuweka mahabusu,”
alisema.
Alisema walikaa rumande kuanzia saa 1:30
usiku hadi saa 4:00 usiku na kuwataka
wajidhamini wenyewe, kisha kuwaachia.
Alisema baada ya kubaini matatizo kwenye
vituo, alilazimika kumpigia simu,
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji Damian Lubuva ambaye ameongeza
mashine 60 za BVR na tayari mashine 25
zimeongezwa maeneo yenye wapiga kura
wengi.
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz
Bano jana alikana CCM kuwatuma vijana
kufanya vurugu vituoni.chanzo:MWANANCHI
Mbunge wa Arusha mjini,Godbless Lema
Post a Comment