Dar es Salaam. Serikali imesema kuanzia
Julai mosi mwaka huu, ajira za utumishi
wa umma zitakuwa zikiombwa kwa njia ya
mtandao, ili kuongeza ufanisi wa mchakato
wa kuwapata watumishi wenye sifa na
kupunguza malalamiko ya kupotea kwa
barua za maombi.
Akizindua baraza la kwanza la wafanyakazi
wa Ofisi ya Rais, Sektretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina
Kombani alisema mtandao huo
umezinduliwa na waombaji watapaswa
kuingia katika tovuti maalumu ya ajira na
kutuma maombi yaliyoambatanishwa na
vyeti vya taaluma walizosomea.
“Maombi kwa njia ya mtandao yatapunguza
kazi ya kuchambua maelfu ya barua za
maombi ya kazi zilizokuwa zinatumwa,
itapunguza pia manung’uniko kwamba
barua zimetumwa kisha zimekaliwa tu,”
alisema Kombani.
Waziri huyo, alisema kwa kutumia
utaratibu huo mpya, wananchi wanaotaka
ajira serikalini watakuwa na uhakika kuwa
barua zao zimefika na kupokewa na
wahusika. Pia, wanaweza kupata mrejesho
kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu zao za
mkononi.
Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier
Daudi alisema baada ya kuona mchakato
wa kuajiri unachangamoto nyingi,
waliamua kubuni mfumo wa kuomba ajira
kupitia mtandaoni.
“Utaratibu huu utatupunguzia gharama,
wanafunzi wanaohitimu kila mwaka
vyuoni ni maelfu kwa maelfu na nafasi
tunazopata serikalini kupitia sekretarieti ya
ajira hazizidi 12,000 kila mwaka,” alisema
Daudi.
Hata hivyo, katibu huyo alisema
wamekuwa wakipata changamoto kubwa
kutokana na baadhi ya waombaji kutumia
vyeti vya kughushi na hivyo kulazimika
kwenda kwenye vyuo husika kuvithibitisha.chanzo:Mwananchi
Waziri wa nchi,ofisi ya Rais (utumishi)
Post a Comment