mwaandishi wetu Kilwa…….
Kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri ya
wilaya Kilwa mkoani Lindi kimeshindwa kuendelea baada ya madiwani kugomea kufanya kikao hicho kwa madai mbalimbali
ikiwemo kushinikiza kulipwa posho zao zaidi ya miezi mitano.
Hali hiyo ilijitokeza
baada ya diwani wa kata ya Kilanjelanje Saidi Mtotela kuomba mwongozo kwa
makamu mwenyekiti ambaye alikuwa anaongoza kikao hicho, juu ya posho , maslai
na stahiki za madiwani.
Baada ya hoja hiyo kujibiwa na Mwanasheria wa halmashauri
hiyo Godfray Jafari kwa kuainisha aina
za posho madiwani waliomtaka kaimu mkurugenzi Peter Mwelekela kutoa maelezo juu
ya madai ya fedha zao za posho za
miezi mitano wanayodai pamoja na kiiunua mgongo chao kabla ya baraza
kuvunjwa.
Abdala Mkumbaru diwani wa kata ya Chumu alisema kuwa hakuna
haja ya kuendelea na baraza kama ofisi ya mkurugenzi haina majibu yakutosha juu
ya malipo ya madeni ya madiwani hao.
Mkumbaru alisema kipindi cha madiwani kuwa madarakani
kimebaki kifupi sana hivyo kama halmashauri hataweza kuwalipa katika kipindi
hiki cha dakika za lala salama hawaweza kuzipata tena fedha
Diwani Haji Mulike alisema madiwani hawako tayari kuendelea
na kikao hicho mpaka mkurugenzi alipe
madai yao katika kikao hicho
ndipo waendeleo kufanya.
Mulike alisema kuwa watendaji wa halmashauri hiyo wamekuwa na
dharau kwa madiwani na kuwasababishia madeni katika taasisi za fedha baada ya
kushindwa kulipa madeni ya mikopo ambapo
kila mwezi ukatwa lakini hazifikishi benki kwa ajili ya kulipa madeni yao.
Alisema kuwa kwa
kipindi cha miezi zaidi ya mitano madiwani wamekuwa wakikatwa fedha za posho
zao kwa ajili ya kulipia madeni ya
mikopo ya zaidi ya shs milioni 43 hazijalipwa hadi sasa.
Kwa upande kaimu
mkurugenzi mtendaji Peter Mwelekela aliwataka madiwani hao kuendelea na kikao
hicho wakati zoezi la kuwalipa madeni yao linashughulikiwa kiutekelezaji.
Kauli hiyo iliongeza vurugu hadi kumlazimu makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bakari Nalinnga kufunga kikao hicho kwa kubadilisha tarehe ya kufanyika tena huku
akiwaangiza watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatafuta majibu na fedha za kumaliza tatizo.
Post a Comment