Mwaandishi wetu Lindi……
Afisa Mfawidhi tume ya haki za
binadamu Kanda ya Kusini Mourice
Chisi amewataka wasaidizi wa kisheria(paraligue) kutumia nafsi zao kuwasaidia wananchi mkoani
Lindi katika kutatua migogoro iliyochini ya uwezo bila kuleta mgongano na
vurugu.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa
anafunga kikao kazi na kugawao vyeti kwa wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya za sita za
mkoa wa Lindi kilichoandaliwa na Kituo cha msaada wa kisheria wanawake na
watoto mkoani Lindi la LIWOPAC.
Chisi alisema kuwa wasaidizi wa kisheria ni
watu muhimu katika maeneo ya vijiji na mjini ambako huduma za
mahakama ziko mbali kwani kutokana uwezo wao na uzoefu, ujuzi
walionao wanaweza kufanya kazi za usaidizi wa kisheria na
kuweza kutataua migogoro mbalimbali katika jamii bila kufikisha
mahakamani.
Nichukue nafsi hii kuwaomba wasaidizi
wa kisheria kuwa waadilifu katika za kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na
migogoro mbalimbali na katika utetezi wa haki za wanawake , watoto na jamii kwa
ujumla, alisema Chisi
Kwa upande wake mratibu Kituo
cha msaada wa kisheria wanawake na watoto LIWOPAC ,Cosma Bulu alisema
kikao hicho ni kikao cha kazi kwa wasaidizi wa kisheria cha
kujadili changamoto na mafanikio yaliyopatikana katika
utendaji kazi na kubadilishana uzoefu.
Bulu alisema kwa kipindi cha mwaka
2013/14 wasaidizi wa kisheria wameweza kufanya kazi mbalimbali
ikiwemo kutatua migogoro ya kijamii na kupunguza wananchi kwenda
mahakamani kudai haki zao kwa kupeleka kesi.
Post a Comment