Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Mwanza – Dar-es-salaam eneo
la kijiji cha Undomo kata ya uchama wilayani nzega mkoani tabora.
Katika ajali hiyo inayodaiwa kuwa chanzo chake ni mwendo kasi na
baadhi ya madereva katika magari hayo kutokuwa makini ambapo basi la
Super Shem lenye nambari za usajiri T874 CWE lililokuwa likitokea
Dar-es-salaam liligongana uso kwa uso na gari aina ya LAND CRUIZER lenye
nambari za usajiri SM 4905 mali ya halmashauri ya wilaya ya nzega
ambapo watumishi watatu wa halmashauri hiyo walifariki dunia.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Patrick Mbozu
anaeleza namna walivyopokea tukio hilo la ajali lililosababisha majonzi
na simanzi
Kaimu mganga mkuu mfawidhi wa wilaya ya Nzega Dr.Erick Mbuguye
anaeleza hali ya majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo na kulazwa.
Post a Comment