Baadhi ya watu wakiamulia ugomvi uliotokea kati ya wanachama na viongozi wao.
Ofisa
wa Ikulu akiwazuia Albino baada ya kutokea mtafaruku na viongozo wao
kabla ya kuingia Ikulu ambapo Rais Kikwete alikuwa na mazungumzo na
baadhi ya viongozi wao.
Watu
wenye ulemavu wa ngozi wakijaribu kutupiana makonde nje ya Ikulu muda
mfupi kabla ya kwenda kuonana na rais jakaya kikwete ambaye alikuwa na
mazungumzo nao.
Na Mwandishi Wetu
WATU wenye ulemavu wa ngozi Albino, leo walizusha vurugu katika viwanja vya Ikulu wakipinga baadhi ya wao kuonana na Rais Jakaya Kikwete.
Kundi la albino waliokuwa wamebaki nje walianza kupaza sauti na kudai waliopewa nafasi ya kuingia kuonana na Mh. Rais si viongozi wao, jambo ambalo liliwalazimu maofisa Usalama kuingilia kati.
Katika
mkutano huo Rais Kikwete alikutana na wawakilishi 15 huku wengine zaidi
ya 30 wakiwa na kuanza kupaza sauti zao na kusema kuwa walioingia ndani
sio viongozi wao kwani muda wao ulishakwisha hivyo ni bora wakatoka
kabla hawajaanzisha vurugu kubwa katika eneo hilo.
CHANZO: HABARI MSETO BLOG
CHANZO: HABARI MSETO BLOG
Post a Comment