0

Rais jakaya Kikwete akizungumza na mlemavu wa viungo ndugu Jivu Bakari Mbunda alipotembelea wilayani Liwale mkoani Lindi
Ni baadhi ya walemavu waliopata msaada kutoka kwa mbunge wao mh.Faith Mitambo

Kwa kutambua umuhimu wa ndugu zetu walemavu uongozi na wananchi wa Wilayani  Liwale mkoani Lindi wamepanga  kuandaa hafla maaalumu na chakula maalumu kwa heshima ya ndugu zetu walemavu ambao watakuwa wageni maalumu na  viongozi ngazi ya wilaya watakuwa ndio wahudumu wao siku hiyo. Hafla hii itafanyika siku ya jumapili ya tarehe 15/3/2015 ambayo itaanza majira ya saa 4.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.
Wote mnakaribishwa na kama una mchango wowote wa kuweza kufanikisha hafla hii utaenziwa kama Sadaka/ ibada kwa wahitaji.

Kauli mbio ya hafla hii inasema PAMOJA TUWAWEZI NDUGU ZETU WENYE ULEMAVU.


Post a Comment

 
Top