0
Wazazi na marafiki wa watahiniwa wakijaribu kuwapa maandishi ya majibu ya mtihani
Udanganyifu wa mtihani umekuwa jambo la kawaida katika Jimbo la India la Bihar lakini picha mpya zimetolewa zinazoonyesha kwamba tukio hilo limefanywa kwa kiwango kikubwa.
Wanafunzi wengi wanasafirisha vitabu vya kusoma na maandishi ya majibu katika chumba hichoo cha kufanyia mtihani licha ya usalama ulioimarishwa.
Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao walipigwa picha wakipanda ukuta wa chumba cha kufanyia mitihani ili wapitishe majibu kwa wanafunzi katika mitihani ya sasa ya shule ya upili.
Mpiga picha Dipankar ambaye alipiga picha hizo katika wilaya ya Saharsa anasema kwamba alipoingia katika chumba cha mtihani na kuchukuwa picha hizo wanafunzi hawakujali.
Licha ya ripoti hizo kutolewa katika magazeti, mamlaka ya maeneo hayo haijachukua hatua yoyote dhidi ya wanafunzi hao, alisema mpiga picha huyo.
 Baadhi ya makaratasi ya majibu ya mitihani yaliokamatwa na maafisa wa polisi
Mtihani huo ulioandaliwa na bodi ya shule ya Bihar (BSEB) ulianza Jumanne na unatarajiwa kuendelea hadi tarehe ishirini na nne mwezi huu.
Viongozi wamesema kuwa zaidi ya wanafunzi millioni 1.4 wanakalia mtihani huo.
Visa vya udanganyifu mwaka huu vimeripotiwa kutoka wilaya ya Saharsa,Chapra, Vaishali na Hajipur.
Magazeti kutoka eneo hilo yamejaa picha za wazazi na ndugu wakipanda katika jengo la shule na kuwapa maandishi ya majibu wana wao kwa lengo la kupita mtihani.
 
Mwanafunzi akitumia karatasi ya majibu kkufanya mtihani
Baadhi ya picha za magazeti hayo zinaonyesha maafisa wa polisi waliowekwa kulinda mitihani hiyo wakichukua hongo.
Dipankar anasema kwamba wakati wa uvamizi huo katika shule moja, mamlaka walikamata makaratasi ya majibu yaliyojaza magunia tisa.
Karibia wazazi ishirini walikamatwa na kuzuiliwa kwa mda mfupi kwa kujaribu kuwasaidia watoto wao kudanganya katika mitihani kabla ya kuwachiliwa baada ya kupewa onyo.

Post a Comment

 
Top