0
Twitter kutochapisha picha za uchi
Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake
katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha Picha
na video chafu.
Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema
''Marufuku kuchapisha picha au video chafu
zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa
bila ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na
picha hizo''
Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa
makosa ya jinai uingereza na Wales.
Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema
watumiaji watakaobainika kukiuka masharti
mapya ''Anuani zao zitafungiwa''
Watumiaji wanaopeleka malalamishi Twitter
kuhusu picha na Video zilizochapishwa
watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia
Kampuni kuwa hawakuwahi kutoa idhini ili
kuchapisha picha au video mtandaoni na
kuonekana kwa hadhira.
Twitter kutochapisha picha za uchi ili
kulipiza kisasa
Yeyote atakayebainika kuchapisha picha hizo
kinyuma na utaratibu wa sheria hii mpya
atatakiwa kufuta kwanza kabla ya kurejeshwa
tena mtandaoni.
Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria
ambayo mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha
mpaka miaka miwili gerezani.
Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa
kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi.
Majimbo kadhaa ya Marekani wameweka
Sheria ya kupambana na vitendo hivi hasa
California,Texas na Utah.
Mabadiliko haya ya twitter yamekuja baada
ya Kampuni hiyo kukosolewa kuwa imekuwa
haifanyi jitihada madhubuti dhidi ya matumizi
mabaya ya mtandao unaofanywa na
watumiaji wake.

Post a Comment

 
Top