0
Alshabaab lavamia mji wa Baidoa
Takriban watu watano wameuawa katika
shambulizi katika makao makuu ya serikali ya
Somalia mjini Baidoa ambayo ni makao ya rais
wa jimbo hilo. Maafisa wa usalama nchini
Somalia wanasema kuwa watu wanaoshukiwa
kuwa wapiganaji wa kundi la Alshabaab
wamepigana na kufanikiwa kuingia katika
makao makuu ya utawala wa jimbo hilo katika
mji wa kati wa Baidoa . Kulingana na waziri wa
usalama katika eneo hilo washambuliaji 3
waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi ya
kikosi cha jeshi la Somalia waliuawa baada ya
majibizano ya risasi ambayo yaliendelea kwa
takriban dakika 20.
Maafisa wawili wa usalama waliuawa huku
raia wawili pia wakijeruhiwa.
Ripoti zinaarifu kuwa mashambulizi hayo
yalianza kwa mlipuko katika lango la makao
hayo kabla milio ya risasi kusikika ndani ya
jengo hilo.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa na shirika la
umoja wa mataifa zimesema kuwa mashirika
mbali mbali yanayotumia jengo hilo
hayakulengwa.
Wanajeshi wa Ethiopia walifanikiwa
kuwafurusha wapiganaji wa Alshabaab katika
mji wa Baidoa mwaka 2012 baada ya
wapiganaji wa kiislamu kuuthibiti mji huo kwa
takriban miaka mitatu.

Post a Comment

 
Top