0
Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani na Paris
St. Germain ya Ufaransa zimesonga mbele
katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya
Klabu Bingwa barani Ulaya kufuatia matokeo
waliyayapata usiku wa kuamkia leo.
Wakicheza kwa kujiamini Bayern Munich
ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali
katika mashandano hayo baada ya baada ya
kuwapa kichapo cha mbwa mwizi wapinzani
wao Shakhtar Donetsk ya Ukrine cha magoli
7- kwa mtungi.
Magoli ya Bayern Munich yalitiwa kimiani na
Thomas Muller, Jerome Boateng ,Franck
Ribery,Holger Bastuber, Robert Lewandowski
na Mario Gotze.
Nayo Paris St. Germain ya Ufaransa imesonga
mbele hatua ya robo fainali baada ya
kuwaondoa Chelsea katika mashindano hayo
japo timu hizo zilitoka sare ya magoli mawili
kwa miwili lakini magoli ya ugenini
iliyoyafunga hapo jana ndio yaliyowanufaisha
Paris St. Germain.
Hivyo mshindi katika mechi hiyo ilibidi
kupatikana katika dakika thelathini za
nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida
kumalizika huku timu zote zikiwa
zimefungana goli moja kwa moja.
Wakiwa na matumaini ya kuingia robo fainali
Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata
goli kupitia Gary Cahill katika 81 lakini Mlinzi
wa zamani wa Chelsea David Luiz akafutilia
ndoto hizo mbali baada ya kusawazisha goli
hilo katika dakika ya 86.
Na hivyo hadi dakika 90 za kwanza
zinamalizika Chelsea 1 na Paris St. Germain 1
na hivyo kulazimika kucheza dakika 30
nyingine ili kumpata mshindi.
Hata hivyo siku ya kufa nyani miti yote
huteleza kwani mbali na Chelsea tena kuwa
wa kwanza kupata goli kwa njia ya penalti
kupitia kwa Eden Hazard katika dakika 96 na
kufufua matumaini ya kusonga mbele, ndoto
hizo tena zilifutiliwa mbali pale mlinzi
mwingine wa Paris St. Germain Thiago Silva
alipopachika goli liliisukumia moja kwa moja
Chelsea nje ya mashindano hay

Post a Comment

 
Top