Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Mdee na wenzake, wanakabiliwa na mashitaka ya kupinga amri halali
ya Jeshi la Polisi na kukusanyika isivyo halali kwa lengo la kwenda
Ikulu.
Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.
Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki, alidai kuwa upande wa
Jamhuri ulikuwa na shahidi mmoja lakini waliiomba mahakama kupanga
tarehe nyingine ya kusikiliza kwa sababu mshtakiwa wa kwanza hayupo na
ushahidi unamzungumzia yeye.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala, alipinga maombi hayo kwamba ushahidi uendelee kusikilizwa.
Upande wa Jamhuri ulidai kesi hiyo haiwezi kuendelea kusikilizwa mpaka mshtakiwa atakapomaliza udhuru wake.
Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni Rose Moshi, Renina Peter
maarufu kama Lufyagila, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fangel,
Edward Julius, Martha Mtiko na Beatu Mmari.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa Oktoba 4, mwaka
2014, katika mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam, walikiuka amri halali
ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi Emmanuel Tille, kwa
niaba ya Jeshi la Polisi.
Pia wanadaiwa siku hiyo walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda Ofisi ya Rais.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment