KIUNGO
Michael Carrick amepata bonge la furaha Manchester United kuelekea
mechi na mahasimu wao wakubwa, Liverpool baada ya kusaini Mkataba mpya
mwaka mmoja Old Trafford.
Taarifa
ya Manchester United iliyotumwa imesema kwamba kiungo huyo
anabaki kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Louis van Gaal licha ya
kukosa miezi miwili na nusu ya kwanza ya msimu kwa sababu ya kuwa
maumivu ya kifundo cha mguu, alichoumia katika mazoezi ya kwanza ya
Mholanzi huyo Agosti mwaka jana.
Van
Gaal amempa Unahodha Msaidizi Carrick, baada ya kiungo huyo kuonyesha
mchezo mzuri na kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Marouane
Fellaini mwishoni mwa wiki katika ushindi wa 3-0 nyumbani dhidi ya
Tottenham kabla ya yeye mwenyewe kufunga.
Michael Carrick ameichezea United mechi 17 msimu huu baada ya kuwa nje mwanzoni mwa msimu kwa sababu ya maumivu ya enka
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 33, aliyejiunga na United kutoka Spurs kwa
ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 18.6 mwaka 2006, alitarajiwa kumaliza
Mkataba wake mwishoni mwa msimu.
Post a Comment