0
WIZARA ya Afya imesema kitengo cha
kutoa huduma za dharura kwa watu
wanaopatwa na ajali za barabarani
kinatazamiwa kuanza kazi mara baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kisasa
lililopo jirani na hospitali ya Mnazi
Mmoja.
Naibu Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit
Kombo alisema hayo wakati alipokuwa
akijibu swali la Mwakilishi wa jimbo la
Kwahani, Ali Salum Haji kutoka (CCM)
aliyetaka kujua lini hospitali ya Mnazi
Mmoja itaanzisha kitengo cha kutoa
huduma za dharura za ajali za
barabarani.
Alisema wizara imeamua kuanzisha
kitengo hicho cha kutoa huduma za
dharura kutokana na kujitokeza kwa ajali
nyingi za barabarani ambazo
husababisha vifo vya wananchi wengi
ambao huhitaji huduma za haraka.
Alisema kwa sasa zipo huduma
zinazotolewa kwa watu wanaopata ajali,
lakini kwa bahati mbaya hakina nafasi ya
kutosha na vifaa vya kisasa vya kutoa
huduma za aina hiyo.
“Mheshimiwa Spika Wiara ya Afya ipo
katika hatua za kuimarisha kitengo cha
kutoa huduma za dharura kwa watu
wanaopata ajali katika hospitali ya Mnazi
Mmoja,” alisema.
Akifafanua zaidi alisema mradi wa
kuimarisha jengo liliopo jirani katika
hospitali ya Mnazi Mmoja la kitengo cha
akinamama wajawazito chini ya ufadhili
wa Serikali ya Uholanzi.
Alisema jengo hilo litakuwa na huduma
za akinamama wajawazito, huduma za
wagonjwa figo pamoja na vyumba vya
dharura kwa watu wanaopata ajali za
barabarani.
Kombo alisema mradi huo upo chini ya
ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na
unasimamiwa na kampuni ya Orio ukiwa
na lengo la kusaidia huduma bora kwa
wagonjwa mbali mbali wanaolazwa katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Post a Comment

 
Top