0

diii
Kocha wa Manchester United baada ya mchezo wao na Arsenal alitoa kauli ya kumtaka kiungo wa timu hiyo Angel Di Maria kuendelea kubaki kuitumikia klabu yake hiyo licha ya kuwepo na maneno mengi kuwa kiwango chake kimeshuka.
Lakini mwenyewe ameibuka na kumtaka wakala wake Jorge Mendes kumtafutia timu nyingine kwa ajili ya kwenda kucheza na yuko tayari kuondoka kwenye klabu hiyo wakati wowote.
Klabu za Barcelona,PSG na Juventus zimeonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ingawa hajafanya nayo mazungumzo yoyote.
Kwa mujibu wake Di Maria amesema amechoka kuitumia klabu hiyo na anatamani kuona akicheza sehemu nyingine.

Post a Comment

 
Top