Mchezaji wa Manchester United Ange di Maria ambaye aliepuka jaribio la wizi nyumbani kwake.
Hatahivyo mbiu ya mgambo ilipigwa kabla ya wezi hao kuingia ndani ya jumba hilo na kulazimika kutoroka.
Tukio hilo lilitokea baada ya Manchester United kuicharaza Leicester City mabao 3-1 katika uwanja wa Old Trafford.
Kiungo
wa kati wa Manchester United Angel Di Maria ndio mwathiriwa wa hivi
karibuni wa wizi wa kutumia mabavu nyumbani kwake huko Cheshire
Uingereza, BBC imegundua.
Baadhi ya wahalifu walijaribu kuvunja
mlango wa nyumba yake katika barabara ya Chelford huko Prestbury siku ya
jumamosi jioni ,maafisa wa polisi wa Cheshire wamesema.Hatahivyo mbiu ya mgambo ilipigwa kabla ya wezi hao kuingia ndani ya jumba hilo na kulazimika kutoroka.
Tukio hilo lilitokea baada ya Manchester United kuicharaza Leicester City mabao 3-1 katika uwanja wa Old Trafford.
Post a Comment